Juni 24, 2026 09:02
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO YAPEWA ELIMU YA RUSHWA

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara Ndugu. Enock Ngailo akitoa Elimu ya masuala ya rushwa kwa watumishi wa Bodi ya korosho Tanzania,mafunzo hayo yalijikita katika kuelimisha na kutambua viashiria vya rushwa na madhara yake katika eneo la kazi na sehemu zingine.

Katika mafunzo hayo,Kamanda Enock ametoa rai kwa wafanyakazi wa Bodi ya korosho kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani jambo hili hudhoofisha utendaji na ufanisi katika kazi lakini pia kuzorotesha ustawi wa uchumi wa Taifa letu.

Related posts

TAARIFA KWA WADAU WOTE WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI/ NOTICE TO ALL STAKEHOLDERS IN THE CASHEWNUT INDUSTRY

Peter Luambano

MKURUGENZI MKUU CBT: KOROSHO MARATHON HUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII, HUTOA FURSA ZA AJIRA

Amani Ngoleligwe

SHILINGI BILIONI 743.57 /= ZAPATIKANA MAUZO YA KOROSHO MSIMU WA 2024/2025

Amani Ngoleligwe