Juni 1, 2025 01:57
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAKULIMA WA KOROSHO MAYANGA AMCOS WAISHUKURU SERIKALI KUWAPATIA PEMBEJEO KWA WAKATI

Baadhi ya wakulima wa zao la korosho kutoka Chama cha Msingi cha Mayanga (Mayanga AMCOS) kilichopo katika kata ya Mayanga mkoani Mtwara, wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia pembejeo za zao hilo kwa wakati muafaka.

Wakulima hao wamesema kuwa upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakati utawasaidia katika uzalishaji kwenye mashamba yao katika msimu wa kilimo wa 2025/2026 na kuongeza matumaini ya kupata mavuno bora na kuwainua zaidi kiuchumi.

Bw. Yusuph Aziz ambaye kwasasa ni mara yake ya tatu kupokea pembejeo za ruzuku katika chama hicho, anasema kuwa alipochukua mara ya kwanza na ya pili uzalishaji wa korosho katika mashamba yake uliongezeka, hivyo katika msimu huu anatarajia kupata mavuno mengi zaidi.

Naye Bi. Asha Issa mkazi wa Mikindani anaishukuru serikali kuwaletea pembejeo wakulima kwa wakati kwani inawaondolea hofu katika uzalishaji wao kutokana na uhalisia kuwa tayari wana uhakika wa pembejeo majumbani mwao.

Utoaji wa pembejeo za ruzuku kwenye zao la korosho ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuinua Tasnia ya Korosho nchini na kuongeza tija kwa wakulima wote wa zao hili Katika kuhakikisha uzalishaji wa zao hili unafikia tani 700,000 msimu wa 2025/2026.

Related posts

ZIARA YA MASOMO YA WANAFUNZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA KILIMO MTWARA-MATI

Peter Luambano

KIKAO CHA SITA CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Peter Luambano

ZOEZI LA UHUISHAJI NA USAJILI WA KANZIDATA YA WAKULIMA LAZINDULIWA RASMI

Peter Luambano