Julai 18, 2026 01:32
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

TIMU YA WAKAGUZI YAKAMILISHA KAZI CBT

Timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma imekamililisha zoezi la ukaguzi katika taasisi ya Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kwa jumla ya hoja kumi (10, zoezi ambalo limefanyika kwa muda wa siku nne kuanzia septemba 19 hadi 22, 2025.

Hoja zilizokaguliwa ni pamoja na Ajira mpya, Upandishwaji vyeo, Mafunzo na maendeleo ya watumishi, Nidhamu, Uzingatiaji wa maadili, Anuai za Jamii, Ufuatiliaji wa usalama na afya mahali pa kazi, Usimamizi wa taarifa, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka, fidia ya magonjwa sugu, na katika hoja hizo, CBT imepongezwa kwa kufanya vema upande wa nidhamu.

Eneo lingine lililofanywa vizuri na CBT ni pamoja na likizo ya mwaka kwa watumishi ambapo watumishi wanaostahili kupata likizo, walipata na walirejea kwa wakati kwenye majumu yao, na taarifa zote kuhusu likizo hufanyiika katika mfumo maalumu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu ndg. Revelian S. Ngaiza, ameshukuru juu ya zoezi hilo na kupokea maoni yaliyotokana na ukaguzi huo pamoja na kuahidi kuyafanyia kazi.

Timu ya wakaguzi hao, imeongozwa na bw. Muhidin A. Muro sambamba na   bi. Hajra H. Mabrouk, bw. Gift S. Lyimo na bw. Florence Mboya.

Related posts

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Peter Luambano

MWONGOZO NA 1 WA USIMAMIZI WA MASOKO NA MAUZO YA KOROSHO GHAFI KUPITIA STAKABADHI GHALANI MSIMU WA MAUZO 2025/2026

Amani Ngoleligwe

HALI YA SOKO LA KOROSHO GHAFI KWA MWAKA 2022/2023

Peter Luambano