Julai 28, 2025 10:12
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MKURUGENZI MKUU CBT ATOA UFAFANUZI KUHUSIANA NA MCHANGO WA ZAO LA KOROSHO KATIKA KUINUA UCHUMI – MTWARA

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania ndg. Francis Alfred amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kufanya jitihada mbalimbali zinazolenga kustawisha tasnia ya korosho nchini pamoja na kuinua uchumi wa wakulima kupitia ruzuku ya 100% ya pembejeo katika zao la korosho ambapo katika kipindi cha miaka minne kiasi cha ruzuku iliyotolewa ina thamani ya shilingi bilioni 626.

Msimu wa 2021/2022 ruzuku ya pembejeo ilikuwa bilioni 59.4; msimu wa 2022/2023 bilioni 96.3; msimu wa 2023/2024 bilioni 189.3 na msimu wa 2024/2025 pembejeo zenye thamani ya shilingi bilioni 281. Hivyo, ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wa korosho imekuwa ikiongezeka kila mwaka.

Ndg Francis amesema kuwa tozo (Halmashauri za Wilaya pamoja na wadau wengine) hulipwa na mnunuzi na siyo mkulima. Wakulima hutozwa kiasi kisichozidi shilingi 100 ambayo hujumuisha gharama za usafirishaji wa korosho na michango mingine ambayo wao wenyewe wamekubaliana katika ngazi ya Kijiji.

Aidha, amesema biashara ya korosho hufanyika kupitia Ushirika na imesaidia kujenga ushirika imara ambapo kwa sasa Vyama Vikuu vya Ushirika vimeanzisha miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa viwanda, ununuzi wa vyombo vya usafiri, ujenzi wa ghala za kuhifadhia mazao nk. Miradi hii inamilikiwa na Wakulima katika maeneo husika na hivyo kukuza uchumi wa wananchi.

Mkurugenzi Mkuu ameyasema hayo Julai 21, 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake – Mtwara ili kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wakielezea taarifa mbalimbali kuhusiana na zao la korosho, ambazo kimsingi zinatofautiana na hali halisi iliyopo.

Related posts

MKURUGENZI MKUU CBT: KOROSHO MARATHON HUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII, HUTOA FURSA ZA AJIRA

Amani Ngoleligwe

BODI YA KOROSHO YATOA JEZI ZA MICHEZO KWA JESHI LA ZIMAMOTO TANZANIA

Peter Luambano

SALES CATALOGUE -TANECU TANDAHIMBA

Peter Luambano