Oktoba 6, 2025 05:09
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATEKELEZA PROGRAMU YA JENGA KESHO ILIYO BORA KATIKA ZAO LA KOROSHO

Bodi ya Korosho Tanzania imetekeleza programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) iliyopo Wizara ya Kilimo katika zao la korosho kwa kuwapatia mafunzo elekezi vijana wahitimu 500 kwenye fani ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali hapa nchini ikiwa ni juhudi za kuendeleza zao hilo.

Vijana hao wamepata mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo katika sekta ya kilimo, hususan kilimo cha korosho, ili waweze kuwa na ufanisi zaidi katika uzalishaji na usimamizi wa zao hilo.

Katika mafunzo hayo, vijana wamefundishwa mbinu bora za kilimo cha zao la korosho, kuwajengea uwezo wa kujua wajibu wao katika tasnia ya korosho ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na ufanisi katika kazi zao na pia wanachangia katika maendeleo ya Nchi.

Vijana hao watakuwa na jukumu la kutoa huduma za kilimo kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya mbinu za kisasa za kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Utekelezaji wa programu ya BBT katika zao la korosho hapa nchini unatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha kipato cha wakulima na kuongeza pato la Taifa kwa ujumla.

Related posts

DKT SERERA AZINDUA MRADI WA GROWING TOGETHER

Amani Ngoleligwe

KOROSHO QUEENS YAPATA UFADHILI WA VIFAA VYA MICHEZO

Peter Luambano

KIKAO CHA KAMATI YA UENDELEZAJI ZAO YA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Peter Luambano