Januari 30, 2026 12:57
Bodi ya Korosho Tanzania
KiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO TANZANIA YASHIRIKI WIKI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA MKOANI PWANI

Bodi ya korosho yashiriki  Wiki ya Uwekezaji  na Biashara Mkoani Pwani iliyoanza  kufanyika octoba 5 na kufikia kilele leo Octoba 10, 2022 katika Viwanja vya Stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mjini ,ikiwa ni maonyesho ya tatu tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo mwaka 2018.
Katika maonyesho hayo washiriki 520 walikadiriwa kushiriki moja kwa moja na watu takribani 15,000 kujionea bidhaa zinazozalishwa kupitia viwanda na fursa zinazopatikana Mkoani humo.
“Maonyesha haya yameratibiwa na TANTRADE kwa kushirikiana na Shirika linalohudumia viwanda vidogo vidogo( SIDO )Kanda ya Mashariki”,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakari Kunenge akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki kufanikisha maonyesho hayo.

Related posts

JARIDA LA KOROSHO MWEZI MACHI 2024

Peter Luambano

Kikao cha 12 cha Bodi ya Wakurugenzi

Peter Luambano

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Peter Luambano