Mei 16, 2024 05:47
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKitelezi

Bodi ya Korosho yawaonya wafanyabiashara wanaozitorosha Korosho nje ya nchi

Bodi ya Korosho Tanzania imewaonya baadhi ya wanunuzi wa zao la Korosho wanaonunua baada ya msimu kufungwa na kutaka kuzitorosha nchini kinyume cha sheria.

Hadi sasa kampuni mbili zimechukualiwa hatua na kutozwa faini ya zaidi ya Sh45 milioni kwa kukiuka taratibu za ununuzi na usafirishaji wa zao hilo.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya uzalishaji wa Korosho msimu wa mwaka 2023/2024, kilichofanyika aprili 7, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tnaznaia Francis Alfred amesema wapo wanunuzi ambao wananunua Korosho baada ya msimu kufungwa na kutaka kuzisafirisha kwenda nje ya nchi kinyume na utaratibu.

Amesema Korosho zinazoruhusiwa kwenda nje ni zile zilizonunuliwa wakati wa minada na zilizobanguliwa kutoka viwanda vya ndani , na zote zinazonunuliwa baada ya minada kufungwa ni kwa ajili ya kubanguliwa na viwanda vya ndani ya nchi tu.

“Hatutoi vibali kwa mtu yeyote wala viwanda, Korosho zilizobaki zitabanguliwa hapahapa nchini, nawatahadharisha wote wanaonunua kinyume cha utaratibu, tutawachukukia hatua kali za kisheria, hata juzi tumekamata gari moja ikiwa na tani 38, wamenunua kinyume cha utaratibu na hawakuwa na vibali”.

“Tumewatoza faini ya zaidi ya Sh25 milioni, pia kuna kampuni moja ilitaka kutorosha Korosho kwenda Dar es Salaam zikiwa hazina vibali, nao tuliwatoza faini ya Sh20 milioni” amesema Alfred

Related posts

WAZIRI WA KILIMO MHE.HUSSEIN BASHE (MB) ASISITIZA ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO NA MWENDELEZO WA UBORESHAJI WA KANZI DATA YA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Peter Luambano

KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUGENZI ROBO YA TATU YA MWAKA

Peter Luambano