Mei 19, 2024 05:55
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKitelezi

WAZIRI WA KILIMO MHE.HUSSEIN BASHE (MB) ASISITIZA ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Akizungumza katika kikao cha tathmini kilichofanyika Jijini Dodoma tarehe 24 April 2023, Mhe. Bashe amesisitiza usajili wa Wakulima kupitia kanzi data ya Wakulima Nchi nzima ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Agenda ya 10/30 ya Kilimo.

Katika kukazia hili,Mhe. Bashe ameiagiza Bodi ya Korosho Nchini kusimamia zoezi hili kikamilifu na kuhakikisha kila Mkulima anaingia kwenye kanzi data,aidha ameongeza kwa kusema, kwasasa hakuna Mkulima wa Korosho atakaepata Pembejeo iwapo hajaingia kwenye kanzi data ya Kilimo.

“Hii itaondoa malalamiko katika zoezi la usambazaji na ugawaji wa ruzuku ya Pembejeo lakini pia usajili huuu utaisaidia Serikali katika jitihada zake za kufanya makadirio ya kuwawezesha Wakulima wa Korosho ili kuongeza uzalishaji na tija katika zao la Korosho”(Mhe.Hussein Bashe).

Related posts

MKUU WA MKOA WA MTWARA AFUNGA MAFUNZO YA UDHIBTI UBORA

Peter Luambano

MAONESHO YA NANENANE 2022-MBEYA

Fesam

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA HUSSEIN BASHE (MB)

Peter Luambano