Disemba 8, 2025 07:28
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAKULIMA WA KOROSHO WAKUMBUSHWA KUHUISHA TAARIFA ZA MASHAMBA YAO.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani machi 8, 2025 wakulima wa zao la korosho wamekumbushwa kwenda kuhuisha taarifa za mashamba Yao katika ofisi za watendaji wa vijiji yalipo mashamba yao.

Hayo yamesemwa na Bi. Mariam Chimbyangu Afisa ugavi na ununuzi wa Bodi ya Korosho Tanzania na mwenyekiti wa wanawake Bodi ya Korosho Tanzania ambaye kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, amewataka wakulima Kwenda kuhuisha taarifa za mashamba yao ili waweze kupata pembejeo za ruzuku zinazotolewa bure na serikali.

Zoezi la kuhuisha taarifa za mashamba ya wakulima linafanyika kila siku ya jumatatu hadi jumamosi kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa11jioni, lilianza rasmi Februari 17, 2025 na linatarajia kukamilika Machi 31, 2025.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yameenda na kauli mbiu isemayo “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” mkoani Mtwara yamefanyika katika viwanja vya Mashujaa Park Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Related posts

HALI YA SOKO LA KOROSHO GHAFI KWA MWAKA 2022/2023

Peter Luambano

WAZIRI WA KILIMO MHE.HUSSEIN BASHE (MB) ASISITIZA ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Peter Luambano

CIAP KUTOKA BURUNDI WAKIWA ZIARANI NCHINI TANZANIA

Amani Ngoleligwe