Aprili 30, 2025 08:03
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MKUU WA MKOA WA MTWARA AFUNGA MAFUNZO YA UDHIBTI UBORA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbasi amefunga mafunzo ya siku tano ya udhibiti ubora wa korosho kwa washiriki 120 yaliyoratibiwa na Bodi ya korosho Tanzania na kufikia tamati tarehe 23 septemba, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa chuo mafunzo ya kilimo MATI kilichopo kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza katika hafla hiyo,kanal Ahmed amesema Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaojihusisha na vitendo viovu vya kuihujumu korosho kwa msimu huu unaotarajia kuanza Oktoba 14, 2022.

Aidha,ametoa wito wa kuongeza mikorosho mipya ili kuongeza tija katika uzalishaji wa korosho na kufikia malengo ya wizara ya kilimo(CBT-Mtwara HQ).

CHUO CHA KILIMO MATI-MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI

Related posts

ELIMU YA MAZINGIRA NA HEWA YA UKAA KWA BODI YA WAKURUGENZI

Peter Luambano

TANGAZO KWA WADAU WOTE WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI

Amani Ngoleligwe

BODI YA KOROSHO YATOA JEZI ZA MICHEZO KWA JESHI LA ZIMAMOTO TANZANIA

Peter Luambano