Oktoba 22, 2025 08:52
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

DKT SERERA AZINDUA MRADI WA GROWING TOGETHER

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji) Dkt. Suleiman Serera, amezindua Mradi wa Growing Together unaofadhiliwa na Serikali ya Kifalme ya Norway kupitia Shirika la Maendeleo la Norway (Norad) wenye jumla ya thamani ya Euro Million 9.5 sawa na Tshs. bilioni 27.8, ambapo hafla hiyo imefanyika tarehe 6 Novemba 2024 katika Hoteli ya Four Points by Sheraton, jijini Dar es Salaam.

Mradi ni wa miaka 5 na umelenga kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs 10), wakulima wadogo 60,000 na wanunuzi wakubwa (Off Takers) 2 kwa mazao ya Mchele, Mahindi, Maharage na Alizeti katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa kutatua changamoto ya tija ndogo, upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wasindikaji na wakulima, mabadiliko ya tabianchi, ajira kwa vijana na wanawake.

Mradi huo unalenga kuongeza tija, kuimarisha upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu, kuimarisha ushirika wa vijana na wanawake na utasaidia wasindikaji na wakulima kulifikia soko la ndani na nje ya nchi na utachangia kufikia malengo ya Ajenda 10/30.

Mradi huo ni mafanikio yaliyotokana na Hati ya Makubaliano (MoU) iliyosainiwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo na Serikali ya Kifalme ya Norway kupitia Wizara ya Mambo na Maendeleo ya Kimataifa ya Norway kufuatia ziara ya kikazi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Norway tarehe 12-14 Februari 2024, ambapo Mhe. Rais alisisitiza utekelezaji wake uwaguse wakulima na wasindikaji nchini.

kwenye MoU iliyosainiwa ikiwemo uwezeshaji wa Sekta Binafsi kuwekeza katika Sekta ya Kilimo kwa kupata mikopo yenye riba nafuu na kuimarisha ushirika wa vijana na wanawake katika Mifumo ya Uzalishaji wa Chakula nchini.

CHANZO: Wizara ya Kilimo

Related posts

SALES CATALOGUE – AGROFOCUS NEWALA

Peter Luambano

Bodi Ya Wakurugenzi Ya Bodi Ya Korosho Imefanya Vikao Vyake Toka 29.10.2021 Na 30.10.2021

Fesam

MKUU WA MKOA WA MTWARA AZINDUA MINADA YA KOROSHO KWA MSIMU WA 2022/2023 LEO TAREHE 21 OKTOBA KWA VYAMA VIKUU VIWILI TANECU NA MAMCU MKOANI MTWARA.

Peter Luambano