Januari 31, 2026 06:28
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

NHIF YATOA ELIMU YA MATUMIZI YA BIMA KWA WATUMISHI CBT

Wataalam kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) septemba 10/2025, wametembelea ofisi za Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) ili kutoa elimu ya matumizi ya bima na namna mtumishi wa Umma anavyonufaika na bima hiyo pamoja na elimu kuhusu kifurushi cha huduma za ziada ambacho watumishi wa CBT wananufaika nazo.

Pamoja na mambo mengine  wataalam hao wameeleza kuwa NHIF imefanya maboresho kadhaa ya mifumo ikiwa ni pamoja na mfumo wa NHIF SELF SERVICE, unaomuwezesha mwanachama mwenyewe kujisajiji na kujitengenezea kadi.

Pia mfumo huo humuwezesha mwanachama kuona michango yake ya kila mwezi, kusajili wategemezi wake na kuwatengenezea kadi za bima ya afya ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi.

Aidha huduma hizo zinazotolewa na NHIF zinapatikana katika hospitali za Umma na binafsi. Wataalam hao ni Muhamed Jabu ambaye ni Afisa Wanachama Pamoja na dkt. Mamiza Habibu ambaye ni Afisa Udhibiti Ubora.  

Related posts

Kikao cha 12 cha Bodi ya Wakurugenzi

Peter Luambano

WAKULIMA RUNALI WAUZA KOROSHO KILO 20,630,516 KWA BEI YA JUU TSH 2,610

Amani Ngoleligwe

BALOZI AVETISYAN ATEMBELEA BODI YA KOROSHO, KONGANI LA VIWANDA MARANJE

Amani Ngoleligwe