Oktoba 5, 2025 11:53
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

VIJANA NA WANAWAKE WAHIMIZWA KUJIHUSISHA UONGEZAJI THAMANI ZAO LA KOROSHO

Vijana na wanawake wa mikoa inayozalisha zao la korosho nchini, wametakiwa kujihusisha katika shughuli za uongezaji thamani wa zao hilo ili kutanua wigo wa matumizi ya korosho na bidhaa zake.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Kanali Michael Mtenjele aliyekuwa mgeni rasmi katika siku ya kula na kunywa vinywaji na bidhaa zitokanazo na zao la korosho maarufu KOROSHO DAY, shughuli iliyofanyika katika viwanja vya maonesho ya nanenane Ngongo- mkoani Lindi Agosti 05-2025.

Pamoja na hayo, Kanali Mtenjele ameitaka Bodi ya Korosho Tanzania na kituo cha Utafiti wa kilimo TARI-Naliendele kuhakikisha kuwa KOROSHO DAY inafanyika kila mwaka ili kuendelea kuhamasisha wananchi wote na wadau mbalimbali kutumia bidhaa zitokanayo na korosho.

Aidha KOROSHO DAY hufanyika kila mwaka katika viwanja vya maonesho ya nanenane, katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, imefanyika Agosti 05-2025 ikiwakutanisha pamoja watumishi wa Bodi ya Korosho Tanzania wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Ndg. Mangile Malegesi pamoja na wadau wengine wa Korosho.

Related posts

KOROSHO MARATHON YAFIKA KILELENI KWA SHANGWE

Amani Ngoleligwe

ZIARA YA MASOMO YA WANAFUNZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA KILIMO MTWARA-MATI

Peter Luambano

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg. Francis Alfred Pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI)-Naliendele Dkt Fortunus Kapinga wamepokea ujumbe wa wageni kutoka Nchini Benin leo tarehe 3 Octoba 2022.

Peter Luambano