Aprili 30, 2025 09:25
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA YAKUTANA NA MENEJIMENTI KATIKA KIKAO CHAKE CHA KWANZA

Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania iliyoteuliwa hivi karibuni ikiongozwa na Mwenyekiti Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce D. Mwanjile ndc imefanya kikao chake cha kwanza Machi 18, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Tanzania uliopo Mtwara Mjini ili kujadili masuala mbalimbali yahusuyo Tasnia ya Korosho.

Katika kikao hicho Menejimenti imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Bodi ya Korosho Tanzania zilizofanyika kuanzia mwezi Julai, 2024 hadi Machi, 2025 na taarifa ya mpango kazi wa robo ya nne kuanzia mwezi Aprili hadi Juni, 2025.

Miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kongani ya viwanda katika Kijiji cha Maranje Kata ya Mtiniko Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara, taarifa ya utekelezaji wa ukarabati wa majengo ya Bodi ya Korosho Tanzania kwa mwaka 2024/2025, taarifa ya utekelezaji wa programu ya Jenga Kesho Iliyobora katika zao la korosho (BBT Korosho) kwa mwaka 2024/2025 na nyinginezo.

Pamoja na mambo mengine Menejimenti imetakiwa kuendelea na usimamizi mzuri wa BBT Korosho kwa kuhakikisha kuwa shughuli zote za kilimo cha zao la korosho zilizopo katika maeneo waliyopangiwa zinatekelezwa ipasavyo. Maafisa kilimo hao ambao idadi yao ni 500 wapo katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Tanga na Pwani, na hivi karibuni Bodi ya Korosho ilizindua ugawaji pikipiki na vishikwambi kwa maafisa kilimo hao ili kuongeza uzalishaji zaidi.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho Tanzania kikiongozwa na mwenyekiti wa Bodi Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce Mwanjile ndc, sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania ndg. Francis Alfred, Bodi ya Wakurugenzi, Viongozi wa kurugenzi, Idara, Vitengo na Matawi yote ya Bodi ya Korosho Tanzania.

Related posts

SILINDE ASHIRIKI COP29 NCHINI AZERBAIJAN.

Amani Ngoleligwe

TANGAZO KWA WADAU WOTE WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI. NOV 11-2024

Amani Ngoleligwe

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Francis Alfred, akizungumza na Wakulima wakati wa ufunguzi wa mnada wa kwanza wa ununuzi wa Korosho Msimu 2023/2024 katika Kijiji cha Mburusa Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara Octoba 20,2023

Peter Luambano