Mei 3, 2024 07:16
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Ni katika mwendelezo wa matumizi ya teknolojia katika Sekta ya Kilimo,Bodi ya Korosho Tanzania imeendelea na utoaji mafunzo kwa viongozi wa AMCOS zote chini ya Vyama Vikuu vya RUNALI,TANECU,MAMCU na TAMCU ili kwenda sambamba na mabadiliko yanayokusidiwa,mafunzo haya ni matokeo ya usajili wa wakulima unaoendelea Nchini nzima kwa Mikoa inayolima Korosho.

Serikali imeweka msisitizo katika matumizi ya teknolojia ili kupata taarifa za wakulima kwa wepesi na haraka, hivyo miongoni mwa mikakati ya kufanikisha dhumuni hili ni matumizi ya Teknolojia inayolenga kuwa na Kanzi data ya wakulima wote Nchini.

Hivyo vyama vya ushirika kwa sasa vinapaswa kuendana na mabadiliko ili kuhudumia wanachama wao kupitia teknolojia,hili litarahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi pia kupunguza migogoro isiyo na tija.

Related posts

BODI YA KOROSHO YAPEWA ELIMU YA RUSHWA

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO NA TARI WAFANYA KIKAO CHA PAMOJA

Peter Luambano

KIKAO CHA NNE CHA BODI YA WAKURUGENZI BODI YA KOROSHO

Fesam