Mei 1, 2025 01:21
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

ZIARA YA MASOMO YA WANAFUNZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA KILIMO MTWARA-MATI

Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo Mtwara wakiwa katika ziara ya masomo ya nadharia Bodi ya Korosho Tanzania,lengo la ziara hiyo ni kujifunza namna Bodi ya Korosho inavyofanya kazi zake hususani upande wa Kilimo.

Katika kufanikisha hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Ndug. Francis Alfred akiambatana na waataalamu wa Idara mbalimbali kwa pamoja wamewezesha ziara hiyo kwa kutoa ufafanuzi mbalimbali na jinsi Bodi ya Korosho chini ya wizara ya Kilimo inavyotekeleza majukumu yake katika kuboresha na kuendeleza Kilimo cha zao la Korosho Nchini Tanzania ikiwa ni sehemu yaa kukuza uchumi wa Nchi.

Akiongea na wanafunzi hao walioambatana na Wakufunzi wao, Mkurugenzi Mkuu amewaasa kuzingatia masomo yao ili kuleta tija ya elimu waipatayo na kuwa na manufaa kwa jamii watakayo kwenda kuitumikia na kuwa mfano wa kuigwa.

Related posts

MKURUGENZI MKUU CBT: KOROSHO MARATHON HUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII, HUTOA FURSA ZA AJIRA

Amani Ngoleligwe

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO YAPOKEA TANI 3,680 YA SULPHUR KUPITIA BANDARI YA MTWARA

Peter Luambano