Januari 18, 2026 12:12
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KIKAO CHA SITA CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce Damian Mwanjile ndc ameongoza kikao cha Bodi ya Wakurugenzi tarehe 19 Oktoba 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Tanzania kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu Mtwara
Menejimenti imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazigo ya kikao kilichopita, taarifa ya utekelezaji wa robo ya kwanza, mipango ya utekelezaji kwa robo ya pili ya mwaka 2022/2023. Pia Bodi imepitia utekelezaji wa maagizo ya viongozi yaliyotolewa huko nyuma ikiwa ni pamoja na maandalizi ya msimu wa mauzo ya korosho ya mwaka 2022/2023.
Akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti amesisitiza kuongeza ufanisi katika kutekeleza shughuli zilizopangwa na kupitishwa ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti ameipongeza Menejimenti kwa uwajibikaji mzuri katika kutimiza majukumu yao ya kazi.

Related posts

MAAFISA KILIMO WATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU UZALISHAJI WA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

BODI YA WAKURUGENZI CBT YAITAKA MENEJIMENTI KUSIMAMIA VEMA TASNIA YA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

TANGAZO KWA WADAU WOTE WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI. NOV 11-2024

Amani Ngoleligwe