Aprili 29, 2024 01:17
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA HUSSEIN BASHE (MB)

Bodi ya Korosho Tanzania yatekeleza agizo la Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe (MB) kwa kutoa vitabu vya kusajili wakulima wa korosho Jimbo la Mtama Mkoa wa Lindi.  Maafisa wa Bodi wametoa mafunzo kwa Maafisa Ugani wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Mtama namna ya kujaza taarifa za wakulima ikiwa na lengo na mwendelezo wa maboresho ya taarifa za awali zilizopo kwenye mfumo wa kidigitali wa usajili wa wakulima(FRS).
Vitabu hivi vimetolewa kwa lengo la kupata taarifa za uhakiki wa usajili uliofanyika awali wa  taarifa za wakulima wa korosho kwani taarifa zao ziko kwenye  mfumo wa FRS uliotolewa na Wizara ya Kilimo.

Related posts

MKUU WA MKOA WA MTWARA KANALI AHMED ABBAS AHMED AZINDUA RASMI KOROSHO MARATHON MSIMU WA PILI 2023

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO YAPEWA ELIMU YA RUSHWA

Peter Luambano

WAZIRI WA KILIMO MHE.HUSSEIN BASHE (MB) ASISITIZA ZOEZI LA USAJILI WA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Peter Luambano