Agosti 1, 2025 03:33
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAKULIMA MNOLELA: TANGU TUANZE KUPOKEA PEMBEJEO ZA RUZUKU MAMBO YANAKWENDA VIZURI SANA

Wakati zoezi la ugawaji pembejeo za ruzuku katika zao la korosho likiendelea katika mikoa mbalimbali inayolima zao hilo nchini, wakulima wa kata ya Mnolela mkoani Mtwara wametoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pembejeo za ruzuku, wakisema kuwa tangu waanze kupata wameona mabadiliko makubwa katika uzalishaji.

Kwa upande wake Hamis Mpinga ambaye ni mkulima kutoka katika Kijiji cha Zingatia anasema kuwa anaishukuru sana serikali kwa kuwaletea pembejeo kwa wakati sahihi. “Tangu tuanze kupata pembejeo uzalishaji unakwenda vizuri, hauna matatizo, nasisi tunafarijika na kazi anayoifanya mama Samia na azidi kuendelea miaka mitano ijayo na nitampa kura yangu”.

Uwesu bin Said, ambaye ni mjumbe wa chama cha msingi cha Mnolela anasema “tumepokea pembejeo na mwaka huu tunaweza kusema kuwa Bodi ya Korosho imetuzidishia, kwasababu chama cha Mnolela kina matawi sita, hivyo wakulima walikuwa wanapata shida kufuata pembejeo makao makuu lakini kwasasa, pembejeo imewafikia wakulima katika maeneo yao yote”.

Naye Afisa kilimo wa kata hiyo kupitia mpango maalum wa Jenga Kesho iliyo Bora Katika zao la korosho (BBT) Benjamin Mwasile anasema kuwa takribani vijiji vyote sita vya kata ya Mnolela wakulima wamepata Pembejeo pia wataalamu wanaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima.

Related posts

Kikao cha ufunguzi wa zoezi la ukaguzi wa hesabu za taasisi Kwa mwaka 2021/2022

Peter Luambano

RAIS DKT SAMIA ASHIRIKI MIKUTANO MUHIMU KUHUSU KILIMO-MAREKANI

Amani Ngoleligwe

BEI YA JUU YA KOROSHO YALETA SHANGWE KWA WAKULIMA KATIKA MNADA WA KWANZA MKOANI MTWARA

Amani Ngoleligwe