Serikali ya jamhuri ya Muunganio wa Tanzania inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kumuinua kiuchumi mkulima wa korosho nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu katibu mkuu (USHIRIKA NA UMWAGILIAJI) Dkt Suleiman Serera (kushoto) wakati wa kikao cha kujadili mfumo wa ununuzi wa korosho na utaratibu a minada kwa msimu wa 2024/25 ijumaa ya septemba 13,2024 katika ukumbi wa Bodi ya korosho Mtwara-Tanzania.
Ameongeza kuwa serikali itaendelea kuboresha kilimo cha korosho nchini kwa kuwapatia wananchi pembejeo na mahitaji mengine ya kilimo pia inaendelea na jitihada za kuwatafuta wawekezaji.
Pia kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya korosho nchini, ndg. Francis Alfred (kulia) amesema kuwa minada ya korosho inatarajia kuanza octoba 11,2024 akisisitiza pia vyama vikuu viweke alama kwenye magunia ya korosho.
Ndg. Alfred amesema kuwa atashirikiana kwa ukaribu na wadau wote wa korosho na kuwa mwendesha ghala yeyote asiyefuata utaratibu atachukuliwa hatua.