Wataalam kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) septemba 10/2025, wametembelea ofisi za Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) ili kutoa elimu ya matumizi ya bima na namna mtumishi wa Umma anavyonufaika na bima hiyo pamoja na elimu kuhusu kifurushi cha huduma za ziada ambacho watumishi wa CBT wananufaika nazo.
Pamoja na mambo mengine wataalam hao wameeleza kuwa NHIF imefanya maboresho kadhaa ya mifumo ikiwa ni pamoja na mfumo wa NHIF SELF SERVICE, unaomuwezesha mwanachama mwenyewe kujisajiji na kujitengenezea kadi.
Pia mfumo huo humuwezesha mwanachama kuona michango yake ya kila mwezi, kusajili wategemezi wake na kuwatengenezea kadi za bima ya afya ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi.
Aidha huduma hizo zinazotolewa na NHIF zinapatikana katika hospitali za Umma na binafsi. Wataalam hao ni Muhamed Jabu ambaye ni Afisa Wanachama Pamoja na dkt. Mamiza Habibu ambaye ni Afisa Udhibiti Ubora.