Novemba 12, 2025 10:11
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MAMCU WAUZA KILO 35,445,155 KWA BEI YA JUU SH. 2,510

Wakulima wa korosho kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU wamefanikiwa kuuza jumla ya kilo 35,445,155 za korosho katika mnada wao wa kwanza uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, mkoani Mtwara. Korosho hizo zimeuzwa kwa bei ya juu ya Sh. 2,510 na bei ya chini ya Sh. 2,310 kwa kilo.

Akizungumza mara baada ya mnada huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Godfrey Malekano, amesema kwamba msimu huu wakulima wameimarika kwa kiasi kikubwa katika suala la ubora wa korosho zao. Ameongeza kuwa matumaini ni makubwa kuona hali ikiendelea kuwa nzuri, hatua itakayowawezesha wakulima kupata mapato zaidi kwa maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, Kaimu Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Robert Nsunza, ametoa wito kwa viongozi wa Ushirika kuhakikisha malipo kwa wakulima yanafanyika kwa wakati stahiki ili kuwaongezea imani na hamasa kwenye uzalishaji.

Hadi kufikia sasa, jumla ya korosho ghafi (RCN) zilizouzwa kupitia minada yote ni kilo 93,879,726.

Related posts

MKUTANO WA 19 WA ACA WA MWAKA NA MAONESHO YA BIDHAA YA KOROSHO NOV 18 – 21 NOV 2025

Amani Ngoleligwe

MWONGOZO NA. 2 WA USIMAMIZI NA UDHIBITI UBORA WA KOROSHO GHAFI WA MWAKA 2023/2024 TOLE0 LA 6

Peter Luambano

JARIDA LA KOROSHO MWEZI MACHI 2024

Peter Luambano