Septemba 13, 2025 12:41
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BALOZI AVETISYAN ATEMBELEA BODI YA KOROSHO, KONGANI LA VIWANDA MARANJE

Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetisyan ametembelea Ofisi za Bodi ya Korosho Tanzania pamoja na eneo la kongani la viwanda lililopo katika Kijiji cha Maranje halmashauri ya mji Nanyamba ikiwa ni njia ya kuendelea kuimarisha Uchumi wa kibiashara hususani katika zao la korosho baina ya mataifa haya mawili.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, amesema kuwa Tanzania na Urusi ni mataifa ambayo yamekuwa na ushirikiano mzuri wa kidiplomasia ambao upo katika Nyanja mbalimbali ikiwamo ya uwekezaji katika kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg. Francis Alfred, amesema kuwa ujio wa Balozi Avetisyan ni fursa kubwa katika kukuza na kupata masoko mapya ya korosho karanga katika soko la Urusi. Licha ya kuwa Urusi hununua korosho katika masoko ya India na Vietnam, lakini wanaweza pia kuja kununua nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha hali ambayo husaidia kuendeleza mipango kwa wakati. Aidha kongani litakapokamilika litakuwa na fursa mbalimbali ikiwamo kuwawezesha wawekezaji kupata maeneo bure kutoa ajira kwa wananchi na nyinginezo nyingi.

Related posts

MKURUGENZI MKUU CBT: KOROSHO MARATHON HUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII, HUTOA FURSA ZA AJIRA

Amani Ngoleligwe

SERIKALI YAJIPANGA KUMUINUA KIUCHUMI MKULIMA WA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

CATALOGUE NO.1 TAMCU

Peter Luambano