Machi 10, 2026 01:57
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAZIRI JAFO AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KUSINI

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Mhe. Dkt. Suleiman Jafo amehitimisha rasmi maonesho ya sikukuu ya wakulima (NANENANE) kanda ya kusini – Ngongo mkoani Lindi.

Dkt. Jafo amepongeza mfumo wa stakabadhi ghalani unaotumiwa na wakulima, mfumo ambao ni wenye tija na unalenga kumnufaisha mkulima na jamii kwa ujumla ikiwamo kutoa ajira.

Aidha wizara ya kilimo imeshika nafasi ya kwanza kwenye maonesho haya kanda ya kusini na kwa upande wa mamlaka za udhibiti, Bodi ya Korosho Tanzania imeibuka mshindi wa kwanza kwenye maonesho haya ukanda wa kusini.

Kwa ukanda wa kusini maonesho haya yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala Agosti 1-2025 na yamehitimishwa rasmi na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Jafo Agosti 8-2025.

Related posts

JARIDA LA KOROSHO MWEZI MACHI 2024

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO YAPOKEA TANI 3,680 YA SULPHUR KUPITIA BANDARI YA MTWARA

Peter Luambano

MAMCU WAUZA KILO 35,445,155 KWA BEI YA JUU SH. 2,510

Amani Ngoleligwe