Juni 16, 2025 08:46
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BOT – MTWARA YATOA ELIMU YA FEDHA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Wataalam kutoka Benki kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara wametoa elimu juu ya alama za usalama zilizoko kwenye noti itolewayo na Benki Kuu ya Tanzania, Utunzaji wa noti na matumizi ya kisasa ya malipo kutumia kadi za benki, kufanya uhamisho (funds transfers) na huduma za mawakala wa huduma za kifedha pamoja na Nidhamu ya Fedha na Matumizi yake na Njia mbalimbali za Uwekezaji sahihi ulio na faida pasipo majanga (risk free).

Wataalam hao wameeleza kuhusu UWEKEZAJI KWENYE HATI FUNGANI (GOVERNMENT TREASURY SECURITIES) ambapo ili uweze kushiriki kwenye uwekezaji wa dhamana za Serikali ni LAZIMA UFUNGUE CDS ACCOUNT inayotolewa na Benki Kuu na ili kufungua CDS account unatakiwa uende kwenye benki yeyote ya biashara hapa nchini hasa benki uliyokwisha kufungua akaunti yako binafsi ukiwa na kitambulisho (NIDA), picha za rangi (Passport size) na TIN number yako.

Vilevile wameeleza kuhusu UTT-Asset Management and Investor Services (UTT-AMIS) ambao ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulioanzishwa na Serikali chini ya Wizara ya Fedha, mfuko huo unatoa fursa kwa wawekezaji wadogo wadogo na wakubwa kuwekeza katika mifuko yao mbali mbali.

Elimu hiyo imetolewa Juni 05, 2025 kwa watumishi wote wa Bodi ya Korosho Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho katika ofisi za makao makuu mkoani Mtwara, ikitolewa na Meneja Huduma za Kibenki Tawi la Benki Kuu Mtwara Ndg. Melchiades Domino Rutayebesibwa sambamba na Ndg. Benny Mgowole na Bi. Neema Nyanda ambao ni Maafisa wa Benki Kuu tawi la Mtwara.

Related posts

RAIS DKT SAMIA ASHIRIKI MIKUTANO MUHIMU KUHUSU KILIMO-MAREKANI

Amani Ngoleligwe

WAZIRI BASHE AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KURUHUSU EXPORT LEVY ITUMIKE KWA WAKULIMA

Amani Ngoleligwe

UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Fesam