Aprili 30, 2025 08:03
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

RC LINDI AZINDUA UGAWAJI PIKIPIKI NA VISHIKWAMBI KWA MAAFISA KILIMO WA BBT-KOROSHO

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telack amezindua ugawaji wa vitendea kazi ambavyo ni pikipiki 152 na vishikwambi 152 kwa maafisa kilimo walioajiriwa na Bodi ya Korosho Tanzania chini ya Mpango wa Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tommorow) BBT wanaofanya kazi mkoani humo.

Mhe. Zainabu amewataka maafisa kilimo hao kutumia vifaa hivyo ipasavyo ili kuleta tija iliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kufufua mashamba pori kwa kuhakikisha kuwa wakulima wanayasafisha mashamba hayo hatua ambayo itapunguza magonjwa na kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania ndg. Francis Alfred amewataka maafisa kilimo hao kusimamia vema ugawaji wa pembejeo za ruzuku zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa wakulima wote wanapata kulingana na stahiki zao ili kuweza kufikia uzalishaji wa tani 700,000 msimu wa 2025/2026 na tani 1,000,000 ifikapo 2030.

Uzinduzi huo umefanyika machi 13,2025 katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa mkoa huo Mhe. Zainab Telack na kuhudhuriwa na viongozi wengine mkoani humo, viongozi kutoka Bodi ya Korosho Tanzania na maafisa kilimo wa BBT.

Related posts

SHILINGI BILIONI 743.57 /= ZAPATIKANA MAUZO YA KOROSHO MSIMU WA 2024/2025

Amani Ngoleligwe

Bodi Ya Korosho Bandarini Mtwara Na Ugeni Toka Zambia

Fesam

TANGAZO KWA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO

Amani Ngoleligwe