Agosti 21, 2025 11:03
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO TANZANIA YAENDELEA NA UBORESHAJI WA KANZI DATA YA WAKULIMA

KILA MKULIMA WA KOROSHO ATAPASWA KUHAKIKISHA KUWA ANASAJILIWA. MKULIMA AMBAYE HATASAJILIWA HATOPATIWA PEMBEJEO KATIKA MSIMU UJAO.
Mara baada ya usajili mfumo utatoa namba maalumu (unique number) kwa kila mkulima ambaye taarifa zake zitakuwa zimehakikiwa. Namba hiyo ndiyo atakayoitumika kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na zao la korosho.
Uzinduzi wa zoezi la usajili utafanyika tarehe 04 Januari, 2023 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Kata ya Naliendele, Mtaa wa Sogea ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Kanali Ahmed Abbas Ahmed. Wageni waalikwa katika uzinduzi huo itakuwa ni pamoja na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Mtwara, Waheshimiwa wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa wa Mtwara, Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Mtwara, Maafisa Kilimo wa Halmasahuri za Mkoa wa Mtwara na Viongozi wa chama. Aidha, Uzinduzi utaendelea kufanyika katika kila Mkoa kadiri ambavyo ratiba itakuwa imepangwa.
Napenda kuchukua fursa kuwajulisha wakulima wote wawe tayari kutoa ushirikiano ili kukamilisha zoezi la usajili kwa ufanisi-Kaimu Mkurugenzi Mkuu,Francis Alfred

Related posts

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UGAWAJI WA PEMBEJEO KWA MSIMU WA 2023/2024

Peter Luambano

TANGAZO KWA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA HUSSEIN BASHE (MB)

Peter Luambano