Aprili 30, 2025 12:28
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BASHE:  BENKI YA USHIRIKA TANZANIA (COOP BANK TANZANIA) KUANZA NA MTAJI WA BILLIONI 55

Benki ya Ushirika Tanzania itaanza na Mtaji wa Shilingi Billioni 55 ikiwa ni Benki ya kwanza nchini inayomilikiwa kwa asilimia 51 na vyama vya ushirika pamoja na wanachama wake na asilimia 49 zinamilikiwa na wadau wengine.

Amesema hayo Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb), wakati akizindua tovoti ya usajili wa washiriki wa tukio la uzinduzi wa Benki hiyo tarehe 10 Aprili, 2025 Jijini Dodoma.

Waziri Bashe amesema kuwa uzinduzi wa Benki ya Ushirika Tanzania (COOP Bank Tanzania) utafanyika tarehe 28 Aprili, 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC), jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Bashe amesema kuwa Benki ya Ushirika itaanza na Matawi manne ambapo ni katika mikoa ya Dodoma, Mtwara, Kilimanjaro na Tabora na awamu ya pili itakuwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya, Mwanza, Dar es Salaam na Katavi.

Kabla ya uzinduzi siku ya tarehe 27 Aprili 2025, kutakuwa na mijadala mbalimbali inayolenga kuendelea kuimarisha Ushirika nchi ambapo wadau takribani 3,000 wakiwemo Watunga Sera, Taasisi za Umma, Sekta Binafsi, Wanaushirika, Wadau wa Maendeleo, Wafanyabiashara, Wawekezaji watapata fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya ushirika.

Kupitia Benki ya Ushirika Tanzania (COOP Bank) wanachama wa ushirika wataweza kupata mikopo nafuu, kuhifadhi fedha salama, na kupata elimu ya kifedha kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na ya kitaasisi.

CHANZO: WIZARA YA KILIMO

Related posts

TANGAZO KWA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

MKUTANO MKUU WA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO 2024

Peter Luambano

WAKULIMA WA KOROSHO WAKUMBUSHWA KUHUISHA TAARIFA ZA MASHAMBA YAO.

Amani Ngoleligwe