Agosti 27, 2025 09:21
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WATUMISHI CBT WAKUMBUSHWA KUJAZA MAJUKUMU YAO KATIKA PEPMIS

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Ndg. Francis Alfred amewataka watumisi wote wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kukumbuka kujaza majukumu yao kwenye mfumo wa Usimamizi na utendaji kazi katika utumishi wa Umma (PEPMIS) ili waweze kupanda madaraja.

Vilevile, amewataka watumishi hao kuheshimiana na kufuata taratibu za kiutumishi wawapo ndani au nje ya ofisi. Ndg. Alfred Ameyasema hayo wakati wa kikao na wafanyakazi wote wa CBT kilichofanyika tarehe 10 Julai, 2025 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za CBT makao makuu, Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara.

Kikao hicho kilichofuatiwa na kikao cha baraza la wafanyakazi kimewakutanisha wafanyakazi wote waliopo Mtwara Makao Makuu na wale waliopo katika matawi yote nchini ambayo ni tawi la Dar es salaam, Mbeya, Katavi, Tunduru, Morogoro, Manyoni, Lindi, Dodoma na Tanga.

Related posts

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Peter Luambano

BASHE AIPONGEZA NMB KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAKULIMA

Amani Ngoleligwe

MIKOA YA KILIMO CHA KOROSHO KUONGEZEKA KUTOKA 5 HADI 18 NCHINI- Naibu Waziri Silinde

Peter Luambano