Aprili 30, 2025 03:34
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

RAIS DKT. SAMIA KUZINDUA BENKI YA USHIRIKA NCHINI

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Benki ya Ushirika (Coop Bank Tanzania), lengo likiwa ni kufufua benki za kijamii zilizofilisika nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari tarehe 10 Aprili 2025 mkoani Dodoma, Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe (Mb) amesema Wizara ilipokea maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, kuhakikisha benki za kijamii zilizofilisika zinarejea na katika hatua za awali mnamo Aprili 28, Rais atazindua Benki ya Ushirika nchini.

Amesema Benki hiyo itazinduliwa ikiwa na matawi manne ambayo yanapatikana Dodoma, Mtwara, Kilimanjaro na Tabora.

“Hatua ya pili itahusisha matawi ya Kagera, Mwanza,Dar es Salaam, Mbeya na Katavi.

“Mafunzo kwa mawakala yanaendelea hivyo mbali na matawi hayo kutakuwa na mawakala nchi nzima na kabla ya uzinduzi mnamo Aprili 28 kutatanguliwa na kongamano la wanaushirikika Aprili 27,”amesema.

Waziri Bashe amesema hatua hiyo ni maelekezo mahususi ya Rais Dkt. Samia kwa Wizara ya Kilimo.

Amesema, Benki nyingi za ushirika zimefilisika na Rais Dk.Samia ameona haja ya kurejesha benki hizo ili kuinua uchumi kwa jamii hususani wa wakulima.

“Lengo hapa ni wakulima na jamii kuwa na benki ambazo zitawasaidia na kuwaondolea adha wanazokutana nazo katika Benki za kibiashara,” amesema.

CHANZO: WIZARA YA KILIMO

Related posts

MIKOA YA KILIMO CHA KOROSHO KUONGEZEKA KUTOKA 5 HADI 18 NCHINI- Naibu Waziri Silinde

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO KUTOA MAFUNZO KWA WAKULIMA WA KOROSHO WILAYA YA BIHARAMULO-KAGERA

Peter Luambano

MKUU WA MKOA WA MTWARA AFUNGA MAFUNZO YA UDHIBTI UBORA

Peter Luambano