Machi 3, 2026 05:50
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MKUTANO MKUU WA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO WAFANYIKA JIJINI DODOMA

Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe amewataka wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania katika kusimamia vema Tasnia ya Korosho ikiwa ni Pamoja na kuhakikisha kuwa Kkuanzia msimu huu maafisa kilimo wa BBT wanakuwepo kwenye vyama vya msingi kusimamia zoezi la ukusanyaji wa korosho za wakulima.

Sambamba na hayo, Waziri Bashe amewashukuru viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na wakuu wa mikoa kutoka katika mikoa inayozalisha zao la korosho kwa kuendelea kushirikiana na serikali kuisimamia vema Tasnia ya korosho hasa pale mifumo inapobadilika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Taanzania ndg. Francis Alfred amesema kuwa katika kuhakikisha ubora wa korosho ghafi zinazosafirishwa, kuanzia msimu huu, wasafirishaji wote kutoka ghala kuu kwenda bandari ya Mtwara au ghala la mnunuzi lililoko Mtwara watatakiwa kusajiliwa na kufahamika na Bodi ya Korosho Tanzania.

Hayo yamejiri wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Tasnia ya Korosho uliofanyika agosti 22, 2025 katika ukumbi wa Morena hotel jijini Dodoma ukiongozwa na Waziri wa kilimo Mhe. Hussein M. Bashe sambamba na naibu Waziri wa kilimo ndg. David Silinde na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwamo wakulima, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa mbalimbali, viongozi wa CCM pia viongozi kutoka taasisi mbalimbali.

Related posts

WAKULIMA RUNALI WAUZA KOROSHO KILO 20,630,516 KWA BEI YA JUU TSH 2,610

Amani Ngoleligwe

WAKULIMA WA KOROSHO MAYANGA AMCOS WAISHUKURU SERIKALI KUWAPATIA PEMBEJEO KWA WAKATI

Amani Ngoleligwe

AFISA KILIMO CBT AKITOA ELIMU KATIKA CHOMBO CHA HABARI LINDI

Amani Ngoleligwe