Novemba 25, 2025 05:17
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

CHONGOLO AZITAKA COPRA, TMX NA BODI YA KOROSHO KUANGALIA MAENEO MENGINE YA KIMKAKATI ILI KUPANUA WIGO WA MATOKEO

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kuangalia maeneo mengine ya kimkakati ili kupanua wigo wa matokeo. 

Amefafanua zaidi na kutolea mfano wa ngano na mafuta ili kupunguza utegemezi wa kuagiza kutoka nje ya nchi.  “Tujenge dhamira ya sera ya kudumu katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati na kuongeza wigo wa masoko ili kulinda uchumi wa nchi,” amesema Waziri Chongolo.

Ameelekeza zaidi COPRA kuangalia mazao ya karafuu na kakao na kuelekeza kwamba Mkoa kama wa Morogoro kupatiwa miche laki 5 ili kuanza kazi ya uzalishaji mara moja. 

“Tutumie ata Vijana wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika msimu ujao ambapo wakiwezeshwa kidogo wanaweza kufikia maeneo mbalimbali kwa kutoa elimu kwa Wakulima,” amesema Waziri Chongolo.

Kwa upande wa Mfumo wa mnada kwa njia ya TEHAMA kupitia Tanzania Mercantile Exchange (TMX) na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Waziri Chongolo amepongeza kazi zao na kusema ili waweze kufanya kazi kwa kimkakati zaidi wanahitaji kuangazia maeneo yenye kuleta tija zaidi kwenye mnyororo wa thamani wa mazao na biashara.

Aidha, ameitaka Bodi ya Korosho kufanya uhakiki wa upulizaji wa dawa kwenye korosho kwa kutumia Maafisa Ugani na Vijana wa BBT-Korosho ili kudhibiti mianya kwa kuongeza tija na matokeo zaidi. 

“Tija inaanza kwenye huduma ya wananchi wetu.  Tukishikamana na kufanye kazi kwa pamoja.  Tuongeze kasi ya kazi, tufanye kwa pamoja na ili kupata tija tunayokusudia kwa haraka,” amesema Waziri Chongolo.

Ameongeza kuwa wananchi wanakuwa kama daraja la kuleta maendeleo kwao hivyo tunawajibika kufanya kazi kwa niaba yao.

Related posts

BODI YA KOROSHO YAPEWA ELIMU YA RUSHWA

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA HUSSEIN BASHE (MB)

Peter Luambano

KABRASHA LA MKUTANO MKUU WA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO 2025

Amani Ngoleligwe