Aprili 30, 2025 03:49
Bodi ya Korosho Tanzania

KUHUSU BODI YA KOROSHO TANZANIA

Fesam

Bodi ya korosho Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo iliyoundwa chini ya sheria ya Tasnia ya korosho Namba 18 ya mwaka 2009 (sura ya 203 ya sheria ya Tanzania) na kanuni zake za mwaka 2010 inayoipa jukumu la usimamizi wa Tasnia ya korosho kwenye mnyororo mzima kuanzia kwa mkulima hadi kwa mlaji wa mwisho.

Maono

Kuwa Taasisi mahiri ya udhibiti kwa ajili ya Tasnia ya korosho, yenye ustawi na endelevu.

Dhima

Kuendeleza, kudhibiti na kusimamia masuala yote yanayohusiana na Tasnia ya korosho kwa ufanisi na kwa  kutenda haki.

This is custom heading element

Maadili na Msingi

1.Kumjali mteja

2.Uadilifu katika utoaji huduma

3.Kutokuwa na upendeleo wa aina yoyote

4.Uwajibikaji wa hali ya juu

5.Kutoa huduma kwa uwazi