Skip to main content
WADAU WA TASNIA YA KOROSHO WAKUTANA KUJADILI FURSA ZA MASOKO ULAYA
29 Jul, 2026
admin
Habari na Matukio

WADAU WA TASNIA YA KOROSHO WAKUTANA KUJADILI FURSA ZA MASOKO ULAYA

Wadau wa tasnia ya korosho kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), wabanguaji wa korosho, TANECU, MAMCU, Chama cha Wabanguaji wa Korosho Tanzania (TACP), pamoja na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Uholanzi, wamekutana katika kikao cha pamoja kilicholenga kujadili fursa za ushirikiano wa kukuza soko la korosho zilizobanguliwa nchini Tanzania.

Kikao hicho kimejikita katika kutafuta njia bora za kuwawezesha wabanguaji wadogo wa korosho kufikia masoko ya kimataifa, hususan soko la Ulaya, kwa kuimarisha ubora wa bidhaa, uzingatiaji wa viwango vya kimataifa na kuongeza ushindani wa korosho za Tanzania.

Washiriki wamejikita katika umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, vyama vya ushirika na wadau wa maendeleo katika kujenga mazingira yatakayowawezesha wabanguaji wadogo kunufaika zaidi na mnyororo wa thamani wa zao la korosho, sambamba na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Kupitia ushirikiano huu, Tanzania inalenga kuongeza mauzo ya korosho zilizobanguliwa katika masoko ya kimataifa, kuongeza mapato kwa wabanguaji na wakulima, pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia ubanguaji na uongezaji thamani wa zao la korosho.

Pia unaweza kutufuatilia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, Instagram na Threads ni @Cashewnutboard, Facebook, LinkedIn na X ni Cashewnut Board of Tanzania, Youtube ni Cashewnut Boardtz na Tovuti ni www.cashew.go.tz

Lebo: