Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CBT Brig. Gen. Aloyce Mwanjile ndc (Mwenye kaunda suti) alipotembelea banda la CBT katika maonesho ya nanene Ngongo mkoani Lindi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce D. Mwanjile, ndc, amewataka wakulima wa korosho nchini kutumia viuatilifu vya maji kwa usahihi na kwa wakati ili kudhibiti magonjwa na wadudu waharibifu wa mikorosho, hatua ambayo itachangia kuongeza tija ya uzalishaji, kuboresha ubora wa korosho na kuongeza kipato cha mkulima